Pata faida kwa neno la leo kutoka latika hadithi ya Mtume Muhammad (S A W)

Amesema Mjumbe wa Mwenyezimungu Rehma na amani zimshukie juu yake.
"Mche Mwenyezimungu popote ulipo, na fuatisha jambo jema pindi utakapokuwa umefanya baya (jema hufuta ovu). Na ishi na watu kwa tabia nzuri". (Hadithi hii imepokelewa na Imam Tirmidhiy)
Maelezo
Tunatakiwa kujua kuwa Mwenyezimungu anatuona popote tuwapo. Na tunatakiwa kumuogopa kila aina ya mazingira tulipo.
Ikitokea kama mwanadamu ameteleza kwa kufanya kosa, haraka unatakiwa kulifuatisha kwa jambo jema. Allaah atakufutia jambo lile baya.
Mashaaallaah
ReplyDelete