Amesema mjumbe wa Mwenyezimungu Rehma na amani zimshukie juu yake
Alama za mtu mnafiki ni tatu.
1. Anapozungumza husema uongo, 2. Na anapotoa ahadi hatimizi, 3. Na anapo aminiwa hufanya khiyana. (Hadithi hii imepokelewa na Imam Bukhari na Muslim)
Maelezo
Unafiki ni sifa mbaya na haitakikani kwa muislamu / muumini kuwa nayo. Hizi alizosema Mtume Muhammad ni dalili za mtu huyo.
Uongo umekuwa ni kawaida katika mtindo wetu wa maisha ya kila siku kanakwamba sio dhambi. Kwakweli ALLAAH atunusuru na hili na mengine yote yanayoashiria unafiki.
Ni vema kujiepusha na sifa hizo.
Allaah ndiye mjuzi zaidi
COMMENTS