Umewahi kujiuliza kuwa ni faida gani utapata kwa kula ndizi? Haya ni majibu sahihi na hizi ni faida 6
Ndizi ni miongoni mwa vyakula maarufu sana katika maisha yetu. Na huliwa katika mifumo tofauti kama vile kupikwa zikiwa mbichi, kupikwa zikiwa mbivu, kuliwa zikiwa mbivu bila kupikwa lakini pia kuchomwa.
Katika baadhi ya maeneo ndizi pia hutumika kutengenezea mikate na hata ugali.
Sambamba na hayo unaweza kujiuliza kuwa ni faida gani nitapata kwa kula ndizi? Makala hii imekuletea majibu ya swali lako.
Na hizi ni faida 6 za kula ndizi
Usighafilike;-
Furaha yetu ni kuona wewe msomaji wetu unasema nini kuhusu blog hii
Tuwekee maoni yako chini kabisa ya chapisho hili katika sehemu ya comment
Endapo utakuwa na utaratibu wa kula ndizi mara kwa mara basi utapata faida hizi;-
1. Ni chanzo kikubwa cha nguvu
Ndizi (mbivu) ina kiwango kikubwa cha glucose ambayo moja kwa moja huingia kwenye damu na kuleta msisimko na kuongeza utendaji kazi wa mwili.
Mara nyingi watu wa mazoezi hutumia sana glucose ili kuongeza nguvu, basi ndizi ina glucose nyingi na ni salama zaidi kwa afya ya mtumiaji.
Soma Faida za kula tango
2. Hulainisha mfumo wa mmeng'enyo
Hapa ni kwa upande wa ndizi mbivu. Kama ambavyo unafahamu ndugu yangu kuwa ndizi ni laini hivyo unapokula ndizi unapokuwa na tatizo la mmeng'enyo wa chakula ukila ndizi tatizo kwisha kabisa.
Matatizo ya mmeng'enyo wa chakula yanawasumbua watu wengi na matokeo yake ni kupata choo kigumu au kutopata choo kabisaaa.
Nimekuwekea makala maalum kwa ajili ya tiba za matatizo hayo.
Soma Chanzo na tiba ya matatizo ya mmeng'enyo wa chakula.
3. Huboresha ngozi
Mbali na kuwa na ladha nzuri, lakini maganda yake pia ni msaada mzuri kwa ajili ya urembo.
Maganda ya ndizi yakisagwa vizuri na maganda ya parachichi na kupakwa kwenye ngozi huipendezesha ngozi yako na kuifanya kuwa nyororo.
4. Kinga dhidi ya vidonda vya tumbo
Hii ni kutokana na kuwa ndizi ina vilainishi na nyuzi nyuzi ambazo hulainisha tumbo na kupelekea kuzuia mikwaruzo kwenye tumbo.
5. Kuondoa kiungulia
Tatizo la kiungulia husababishwa na asidi mwilini. Ndizi ni tunda ambalo halina asidi kwa wingi.
Hivyo ndizi ni msaada mkubwa wa tatizo hili hasa ndizi mbivu
Jenga utaratibu wa kula ndizi mbili mbivu kila siku kuepukana na matatizo hayo.
6. Husaidia wagonjwa wa anaemia
Ndizi zina madini ya chuma ambayo huwasaidia wagonjwa wa anaemia. Madini ya chuma husaidia uzalishaji wa madini ya haemoglobin.
Anaemia kitaalamu ni ugonjwa unaosababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini.
Faida ni nyingi lakini hapa tumegusa hizi 6 muhimu. Umefaidika japo kidogo sio?
Basi tunashukuru sana kwa uwepo wako hapa. Kama una faida nyingine unahisi tumeiacha basi tuwekee hapo chini kwenye comment.
Asante sana na Mungu akubariki
************
vizuri sana
ReplyDelete