SABABU 10 KWANINI BLOG YAKO HAINA WATEMBELEAJI? - NINI CHA KUFANYA?

Maoni yako ni ya thamani kwetu kuliko unavyodhani. Tuandikie hapo chini baada ya kumaliza kusoma makala hii itakayokunufaisha


Ni pale ambapo unashangaa kila ukiweka chapisho katika blog yako unaishia kusoma mwenyewe. 

Unaingia kwenye google analytics unakuta mtumiaji ni mmoja au wawili, basi utapata watembeleaji wengi sana siku hiyo hawazidi kumi.

Unakuna kichwa, unainama unatafakari mwisho wa siku unakosa jibu na kutamani kuacha kufanya blogging kabisa. Lakini kwa kuwa ni hobby yako unaona uendelee hivyo hivyo. Kila ukijiuliza nini shida unakosa jibu kabisa.

Unabaki na swali "Kwanini blog yangu haina watembeleaji?"

Haya hapa majibu sahihi  na suluhisho lake. Sababu 10 kwanini Blog yako haitembelewi?


10. Wasomaji hawavutiwi na machapisho yako

Jifanye wewe ndiye msomaji wa blog fulani. Umekuta chapisho ambalo halijakuridhisha. Je? Utarudi tena?

Unadhani nini kitatokea endapo wasomaji hawatavutiwa na kile ulichowabariki? Jibu ni kwamba nao hawatorudi tena kwenye blog yako.

Kama unahisi hilo ndio kikwazo kwako basi fanya mambo haya mawili.

i) Tafuta watu sahihi

ii) Waandikie kile kinacho wahusu

Kikuba ninachokusisitiza hapa ni kuwajua watembeleaji wako kwanza kabla ya kuweka chapisho lako.

Ukiwa mvivu katika hili endelea kutegemea blog yako kutotembelewa.


09. Machapisho yako yana mwisho

Umewahi kutafuta maudhui flani mtandaoni na ukayakuta yalishachapishwa kwa miaka kadhaa nyuma? Haya ndio machapisho yasiyo na muda maalum.

Kwa mfano makala za afya na kilimo ni vitu vya kila siku na vitaendelea kuwepo zama na zama kwasababu kila siku watu wanaumwa na kila siku watu wanalima.

Tofauti na vitu vinavyotamba kwa muda mfupi kama vile habari za mastaa na umbea wa mjini huwa havidumu.

Kama unataka kuwapata watembeleaji kwa muda wote ni kujikita zaidi katika machapisho ambayo yanaishi.

Haina maana kwamba machapisho ya muda mfupi hayatakiwi, ila unaweza kufanya hivi - Katika machapisho 10 basi mawili unaweza kuyaweka yawe ya muda mrefu ambayo unaweza kushea muda na wakati wowote.


08. Unaogopa kutangaza post zako

Waswahili walisema "Woga wako ndio umasikini wako"

Blog ni bidhaa, na bidhaa bila matangazo ni bure. Kuna watu wanasubiri uwajuze kile unachokifanya ili kiwasaidie.

Hutakiwi kusita kutangaza blog / machapisho yako katika mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter, instagram na kadhalika.

Watu watanichukuliaje?

Unaogopa kutukanwa? Unaogopa kusemwa vibaya?

Kuanzia sasa acha kuwaza mambo hayo. Fahamu kuwa kila safari ya mafanikio haikosi changamoto, na kutukanwa na kusemwa vibaya ni miongoni mwa changamoto za kazi hizi.

Cha kufahamu ni kwamba - Blog ni yako, na maudhui ni yako. Kama mtu ataweka komment ambayo haijakupendeza unaweza kuifuta au kukaa kimya tu.


07. Hutumii vizuri SEO

Hii inaitwa Search Engine Optimization. Ni utafutaji maudhui kwa injini pekuzi kama vile google, yahoo, bing na kadhalika.

Tunafahamu kuwa kila siku watu wanatafuta maudhui hasa google, sasa unatakiwa kufahamu kuwa watu wanatafuta nini zaidi ili uweze kuwawekea na wewe kuwa suluhisho kwao.

Tumia mtandao wa google trends ili kujua ni vitu gani vimetafutwa zaidi kwa kipindi fulani.

Ukiyafahamu vizuri yanayotafutwa na watu ni rahisi kuwapata watembeleaji 'organic traffic' ambao ndio miongoni mwa watembeleaji muhimu zaidi wanaotakiwa zaidi na bloggers.


06. Huna ushirikiano na Bloggers wengine

Umekuwa mbinafsi ndio maana blog yako haina watembeleaji.

Ubinafsi upo wa aina nyingi miongoni mwao ni kama vile;-

i) Kutowashirikisha rafiki zako (blogging wenzako) katika kile unachokifanya na kupata ushauri.

ii) Husomi machapisho ya bloggers wengine na kupata muangaza katika kile wanachokifanya.

Jirekebishe katika kasumba hizo mbili utaweza kupiga hatua kubwa na kuwavuta watembeleaji.

Tembelea blog za watu wengine jitambulishe kuwa wewe ni mchanga na uommbe ushirikiano kwao na watembeleaji wao.


05. Vichwa vya habari vibaya

Hebu tazama vichwa vya habari vya post zako. je? Vinaweza kumvutia mtu kufungua post yako?

Kichwa cha habari ndicho hasa humfanya mtu kuifungua habari husika. 

Unapomaliza kuandika chapisho lako andika vichwa vya habari vingi kisha unaweza kuwashirikisha wataalamu kuchagua ni kipi kichwa bora.

Ni vizuri kuandika kichwa cha habari ambacho ni kifupi na chenye namba au idadi. Mfano "Mambo 20 yatakayokushangaza katika usafiri wa ndege"


04. Hujawekeza muda

Kazi ya blogging inahitaji muda wako wa kutosha ili kuandaa kitu ambacho wafuasi wako watapenda.

Haina maana kuwa siku yote uimalizie katika kuandika makala "HAPANA" Lakini unatakiwa kutenga mda maalum ambao akili itakuwa imetulia na kuaanda jambo zuri.

Kama kweli unafanya kwa nia hutakiwi kudharau katika rasilimali ya  muda.


03. Unaogopa kuwekeza gharama stahiki

Blogging ni bure!!

Ni kweli lakini blog bora haiwezi kuwa bure. Blog ni lazima iwe na domain nzuri kama vile mrbunduki.com na nyinginezo.

Lakini pia wekeza zaidi katika kupata template nzuri ambayo itamfanya msomaji afurahie kusoma machapisho yako katika kifaa chake.

Tafuta template ambayo itakuwa rafiki kwa watumiaji wa simu (ambao ndio wengi), lakini pia tablet na kompyuta.

Mbali na gharama hizo pia ni lazima uhakikishe unawekeza katika baadhi ya vifaa kama vile camera na vinavyoendana kama unablog kuhusisha zaidi picha. 

Lakini pia lazima uwe na laptop nzuri na yenye uwezo ili ufurahie uandishi wako pale unapoamua kufanya kazi.


02. Huwashirikishi watu chapisho lako

Kama hujaweka icon za kuweza kushea na kushirikishana makala yako unategemea nini?

Mtu anaweza kupitia machapisho yako na akatamani elimu ile amshirikishe mwenzake, lakini anaposhuka chini haoni mahala ambapo ataweza kupata msaada, atakachokifanya ni kuondoka katika ukurasa huo.

Lakini pia lazima uwakumbushe watu kuwashirikisha wengine. Hii husaidia sana watu kukufahamu na kuyafahamu yale unayoyafanya katika blog yako.


01. Blog yako ni mbaya

Hakuna kitu ambacho kinawakinaisha watembeleaji wa blog kama muonekano na mtindo wake.

Kamwe mtu hawezi kung'ang'ana kuwepo katika blog yako wakati haimpendezi.

Hati mbaya, picha au video mbaya na matangazo yasiyo na mpangilio ni kikwazo sana kwa watembeleaji na huwakwaza sana.

Hebu tazama muonekano wa blog hizi mbili hapa chini. Je? ni sawa

 


NENO LA MWISHO

Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo yanaifanya blog yako kutopata watembeleaji.

Epuka haya kisha utanishukuru baadaye.

Asante kwa kuwa nasi, usisahau kushea makala hii na mwenzako ili aipate elimu hii.

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: SABABU 10 KWANINI BLOG YAKO HAINA WATEMBELEAJI? - NINI CHA KUFANYA?
SABABU 10 KWANINI BLOG YAKO HAINA WATEMBELEAJI? - NINI CHA KUFANYA?
Maoni yako ni ya thamani kwetu kuliko unavyodhani. Tuandikie hapo chini baada ya kumaliza kusoma makala hii itakayokunufaisha
https://1.bp.blogspot.com/-9RDlZjds0w0/YDeKLdBTicI/AAAAAAAAdno/UT-z6rqey1ofVDaENLU8yc43G5ZtF1TJwCLcBGAsYHQ/w243-h158/reason%2Bwhy.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-9RDlZjds0w0/YDeKLdBTicI/AAAAAAAAdno/UT-z6rqey1ofVDaENLU8yc43G5ZtF1TJwCLcBGAsYHQ/s72-w243-c-h158/reason%2Bwhy.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2021/02/sababu-10-kwanini-blog-yako-haina.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2021/02/sababu-10-kwanini-blog-yako-haina.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content