SIRI 6 USIZOZIFAHAMU ZINAZOPATIKANA KATIKA BAMIA

Fahari yangu ni kukuona wewe unasoma makala hii. Unaweza kuwasiliana nami kwa namba 0625 718040

Kama kuna kiungo / mboga maarufu katika jamii yetu haswa uswahilini basi ni bamia. 

Ingawa inaonekana kuwa ni mboga ya watu wa hali ya chini lakini manufaa yake ni makubwa mno.

Bamia ni kiungo maarufu sana katika mchuzi, na kiukweli hunogesha haswaa mboga kiasi cha kuwafanya watu kujiramba kwa utamu.

Mbali na utamu wake lakini unafahamu faida unazozipata kwa kula bamia? Basi kama ulikuwa hufahamu, makala hii itakuwa ni msaada kwako kwani utapata faida kubwa.

Sitaki kukuchosha, zipo faida nyingi lakini hapa nimekuwekea faida 6 tu zitakazo kusaidia milele.


1. Husaidia katika mzunguko wa hedhi

Kuna baadhi ya wanawake wanapoingia katika siku zao za hedhi kuwa siku zao hazitabiriki, kuzidi siku za kawaida au kuvurugika (kuingia na kukata kisha kuingia tena)

Ulaji wa bamia mara kwa mara ni tiba ya tatizo hilo na kurudi katika mzunguko wa kawaida kama inavotakiwa.


2. Husaidia kwenye mwenye pumu

Ulaji wa bamia huongeza kinga ya mwili. Na kwa kawaida mtu akiwa na kinga ya mwili iliyo madhubuti hawezi kushambuliwa na maradhi mara kwa mara.


3. Msaada kwa mwenye vidonda vya tumbo

Inatumia kusawazisha asidi tumboni. Hivyo kwa wenye vidonda vya tumbo ni msaada mkubwa anapokula bamia mara kwa mara.

Soma Faida 7 za kula nyanya chungu (Ngogwe)


4. Huzuia ugonjwa wa kisukari

Fahamu kuwa mlaji wa bamia anakuwa mbali na hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari kwa sababu ya uwezo wake wa kusaidia kuyeyusha au kumeng'enya sukari.

Uyeyushwaji sawia wa sukari mwilini huepusha ugonjwa wa kisukari na hata magonjwa ya moyo.


5. Kusaidia mmeng'enyo wa chakula

Bamia inapoliwa mara kwa mara husaidia kurekebisha mfumo wa umeng'enyaji chakula na kumuondolea mtu matatizo ya kutopata choo au choo kigumu.

Soma pia Tiba rahisi ya mmeng'enyo wa chakula


6. Husafisha damu

Faida nyingine ya ulaji wa bamia ni kusaidia mwili kusafisha damu, lakini pia sambamba na hilo pia bamia husaidia kuondoa sumu mwilini.

Kama tunavyofahamu kuwa miili yetu imetawaliwa sana na sumu kiasi cha kusababisha magonjwa mbali mbali.

Hapa chini nimekuwekea makala ambayo itakusaidia kuondoa sumu mwilini.

Soma makala hii Njia 8 salama za kuondosha sumu mwilini

Nadhani umefaidika kupitia makala hii. Anza sasa utaratibu wa kula bamia walau mara 2 au 3 kwa wiki.

Kama utakuwa na maoni tuandikie hapo chini sehemu ya COMMENT nasi tutayasoma ndani ya muda mfupi.

COMMENTS

BLOGGER: 1


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: SIRI 6 USIZOZIFAHAMU ZINAZOPATIKANA KATIKA BAMIA
SIRI 6 USIZOZIFAHAMU ZINAZOPATIKANA KATIKA BAMIA
Fahari yangu ni kukuona wewe unasoma makala hii. Unaweza kuwasiliana nami kwa namba 0625 718040
https://1.bp.blogspot.com/-sF6mtXPJNeI/YBvG18KLd6I/AAAAAAAAb7M/hie3TP1e-YU0LMf7W_HwuoKBoTi5wk_6ACLcBGAsYHQ/s320/shutterstock_357381095-e1452193160280.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-sF6mtXPJNeI/YBvG18KLd6I/AAAAAAAAb7M/hie3TP1e-YU0LMf7W_HwuoKBoTi5wk_6ACLcBGAsYHQ/s72-c/shutterstock_357381095-e1452193160280.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2021/02/siri-6-zinazopatikana-katika-bamia.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2021/02/siri-6-zinazopatikana-katika-bamia.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content