Maishani matukio ni mengi. Lakini kuna baadhi ya matukio ambayo ni ngumu kuyasahau na hili ni moja wapo

Lengo ilikuwa ni kwenda shambani kwetu na kuchukua mahindi mabichi kwa ajili ya chakula.
Wakati tunarudi kutoka shambani, nilipotazama juu ya mti nilimuona ngedere mmoja akiwa amenikazia macho sana. Sikuwa na wasi wasi sana kwa sababu wanyama wale tumewazoea kiasi kikubwa katika mashamba yetu kwani ni miongoni mwa wanyama waharibifu wa mazao.
Kitu ambacho kilinishitua ni kuona yule ngedere akishuka chini kwa kasi ya ajabu.
Ibrahimu alikuwa ametangulia mbele kiasi cha takriban mita 30 hivi. Mimi nilikuwa nyuma nikiwa nimebeba kikapu ambacho kilikuwa na mahindi, maembe na mapapai.
Nakuja kushituka bwana ninamuona yule ngedere ananikimbilia kwa kasi ya ajabu sana, niliogopa na kutaka kukimbia.
Kabla sijakimbia alinidandia begani na kunata katika bega langu la kushoto. Nilipiga kelele na kuanza kukimbia naye.
Ibrahimu aliposikia kelele zile naye alikimbia sana.
Nilijitahidi kumtupa chini na alipodondoka bado aliendelea kunikimbiza. Baada ya hatua kadhaa alisimama na kurudi. Niliogopa sana kwakweli kwani sikuwahi kuwaza kitu kile.
Nilipowasimulia watu tukio lile
Baadhi yao hawakuamini, wengine walisema kuwa ni imani za kishirikina, na wengine walisema kuwa ngedere yule alikuwa amezidiwa na njaa kiasi cha kuamua kutaka kupora watu mazao.
Baada ya siku kadhaa tulipata taarifa ya kufukuzwa kwa mtu mwingine tena na yeye alibahatika kuporwa matunda ambayo alikuwa amebeba.
Baadaye ngedere yule aliwindwa na kuuwawa kwa bunduki na wazee wa kijiji.
Ukweli ni kwamba
Ngedera yule kumbe hakuwa wa kawaida alikuwa anahusiana sana na mambo ya kichawi.
Tukio hili lilitokea mwaka 2002 wakati nikiwa darasa la tano huko Kijijini Mkalamo Pangani Tanga.
COMMENTS