SITOSAHAU SIKU NILIPOVUNJIWA NYUMBA NA KUIBIWA BAISKELI YA WATU

Mji wa Pangani ni sehemu ambayo nilikuwa nikipata masomo yangu ya sekondari (O Level)

Sambamba na masomo hayo lakini pia nilijiunga na madrasa ya Bakwata na kuanza kusoma na baadaye kusomesha baadhi ya wanafunzi ikiwemo wamama.

Sheikh Ally Jumaa Luwuchu ndiye alikuwa Sheikh wetu na msimamizi wa Madrasa hivyo kwakuwa mimi nilikuwa ni miongoni mwa vijana wake alikuwa anapoondoka na familia yake ananiacha nyumbani ili niwe muangalizi.

Siku hiyo nikiwa nimelala fofofo, mara nikasikia kwa mbaali kelele za watu wakifukuza mwizi mtaa wa pili.

Nilipoamka na kuwasha taa, nashtuka naona mlango uko wazi na wakati niliufunga.

Nilichanganyikiwa sana kwani mpaka hapo ni ishara kuwa nimeshaibiwa.

Niliamua kutoka nje na kuungana na baadhi ya majirani ambao walikuwa wakitafakari juu ya mahala ambako mwizi ameelekea. (Hakujulikana alitokomea wapi)

Niliporudi ndani na kuangalia vizuri nikagundua kuwa baiskelia mbayo ilikuwepo pale pembeni haikuwepo tena (Imeibiwa)

"Daah wameniibia baiskeli aloo" Nilisema peke yangu kwa sauti kubwa kanakwamba nilikuwa na mwenzangu.

Nilitoka tena nje kuwaambia majirani juu ya uhalifu ambao nilifanyiwa na wale wezi. Hakuna ambaye alikuwa na msaada zaidi ya kunipa pole tu.

Kulipopambazuka sheikh alipigiwa simu na alikuja jioni. Niliogopa sana kwani Mzee angenifikiriaje kwa tukio lile?

Lakini hakunigombeza wala kunifokea bali alisema kuwa nisiwe na wasi wasi ni  mambo ya kawaida na nijitahidi kuwa muangalifu.

"Mungu ampe maisha marefu Sheikh wangu ambaye kwa sasa ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga"


Polisi walitaka kunikamata

Jioni ile nikiwa nimekaa pale nyumbani ghafla lilikuja pira la polizi na kunitaka niende polisi kwa ajili ya kutoa maelezo juu ya uhalifu ambao umetendeka pale.

Hatukujua ni nani alipeleka taarifa ile polisi. Lakini Sheikh alinambia kuwa usiende kokote watakusumbua tu.

Hii ilikuwa ni mwaka 2007 nikiwa kidato cha Tatu katika shule ya Sekondari ya Funguni - Pangani Mjini.

COMMENTS

BLOGGER: 2


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: SITOSAHAU SIKU NILIPOVUNJIWA NYUMBA NA KUIBIWA BAISKELI YA WATU
SITOSAHAU SIKU NILIPOVUNJIWA NYUMBA NA KUIBIWA BAISKELI YA WATU
https://1.bp.blogspot.com/-l_vpQdUNZJs/YDEYe5H16GI/AAAAAAAAdbM/XMmlv7qqNOgvl_MO6OPPOZemfiI2c2kVwCLcBGAsYHQ/s320/unnamed.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-l_vpQdUNZJs/YDEYe5H16GI/AAAAAAAAdbM/XMmlv7qqNOgvl_MO6OPPOZemfiI2c2kVwCLcBGAsYHQ/s72-c/unnamed.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2021/02/sitosahau-siku-nilipovunjiwa-nyumba-na.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2021/02/sitosahau-siku-nilipovunjiwa-nyumba-na.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content