LIFAHAMU ENEO LA KIJUNGU MKOANI MBEYA NA MAAJABU YAKE

Vivutio vya watalii ni vingi, huwa tunakusogezea kimoja baada ya kingine. Eneo hili linaitwa Kijungu (Mkoani Mbeya)

Kijungu ninini?

Kijungu ni shimo kubwa lenye mfano wa bakuli au chungu ambalo maji mengi huporomoka na kuingia hapo kabla ya kutokea upande wa pili.

Kutokana na umbo lake ambalo limefanana sana na chungu,  ndio sababu ya kuitwa kijungu.

Historia yake

Hapo kale nyuma kidogo ya eneo la kijung kulikuwa na mwamba ambao unazuia maji kupita, maji yale yalikuwa yakiruka na kutua sehemu ya mbele ndio pakachimbika na kutengeneza eneo hilo.

Lakini mbali na hayo hii ni sehemu yenye masharti sana katika mila za kabila la wanyakyusa.

  • Pembeni ya eneo hilo kuna kidaraja chembamba ambacho wenyeji walikuwa wakikitumia kwa kuvuka kwenda upande wa pili. Na kuvuka hapo kuna masharti yake. Ukitoka upande mmoja unatanguliza mguu wa kulia na ukitoka upande mwingine unatanguliza mguu wa kushoto.
  • Itikadi zinasema kuwa, lile ni eneo la mizimu. Kama unavuka na mzigo wa chakula kama vile mahindi, mihogo, ndizi au kingine chochote ni lazima kwanza utupe chakula hicho kidogo kabla ya kuvuka. Laa sivyo chakula hicho kitaanguka na hutofanikiwa kuvuka nacho (Itikadi za kimila.
  • Maji yanapoingia kwenye kijungu hutokea mbele upande wa pili. Lakini wazee wanasema kuwa kabla maji yale hajatokea pale husafiri kwanza upande wa kilomita 2.5 chini ya mlima huko na kurudi kisha ndipo hutokea pale.
  • Ikitokea mtu amezama pale kwenye kijungu basi ataonekana baada ya siku 7 akiwa tayari ameshakufa.
  • Mwamba wa eneo lile unateleza na ni hatari kwa watalii ambao wanatembelea na kupiga picha. Usipokuwa makini unaweza kujikuta umetumbukia ndani na kupotea.
  • Huruhusiwi kuogelea mahala pale kutokana na hatari iliyopo.
  • Unaruhusiwa kupiga picha na video.
Ukishuka chini ya mto ule unakutana na daraja la Mungu. Hili ni daraja la asili ambalo lipo hadi leo na lilitumika sana kipindi hicho cha nyuma na wakazi wa pale.

Yako mengi ambayo tulijifunza na kujua historia ya eneo lile la kijungu. Hayo ni baadhi tu.

Tunaomba maoni yako chini hapo utuambie kuwa ni mahala gani ungependa tukuletee historia yake?

Asante kwa kuwa nasi

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: LIFAHAMU ENEO LA KIJUNGU MKOANI MBEYA NA MAAJABU YAKE
LIFAHAMU ENEO LA KIJUNGU MKOANI MBEYA NA MAAJABU YAKE
Vivutio vya watalii ni vingi, huwa tunakusogezea kimoja baada ya kingine. Eneo hili linaitwa Kijungu (Mkoani Mbeya)
https://1.bp.blogspot.com/-PIcOLiDMzFw/YD5pL58bXRI/AAAAAAAAeIM/XCGdl-EqZ-kAVGfF0RzjS2jbZxAc1u9PACLcBGAsYHQ/s320/IMG_20210228_142635_531.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-PIcOLiDMzFw/YD5pL58bXRI/AAAAAAAAeIM/XCGdl-EqZ-kAVGfF0RzjS2jbZxAc1u9PACLcBGAsYHQ/s72-c/IMG_20210228_142635_531.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2021/03/lifahamu-eneo-la-kijungu-na-maajabu-yake.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2021/03/lifahamu-eneo-la-kijungu-na-maajabu-yake.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content