MAMBO USIYOYAFAHAMU KUHUSU DARAJA LA MUNGU MBEYA

Vivutio vya watalii ni vingi, huwa tunakusogezea kimoja baada ya kingine. Hili ni Daraja la Mungu Mkoani MBEYA

 

Dunia na maajabu yake.

Kila sehemu ina historia yake,  lakini baadhi ya historia hustaajabisha sana.

Umeshawahi kulisikia daraja la Mungu?

Bunduki Media ilifunga safari mpaka eneo hilo la kihistoria.

Pichani ni Mwandishi Saidi Bunduki na nyuma ni Daraja hilo.

Hili ni daraja la asili ambalo hupatikana katika Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Takriban kilomita 65 kutoka Mjini Mbeya kuelekea barabara iendayo Kyela,  unashukia katika Kijiji kinachojulikana kwa jina la KK (Kijiji Kitulivu).

Unaacha barabara kuu na kuingia barabara ya vumbi upande wa kulia. Mwendo wa takriban dakika 20 ukiwa kwenye piki piki. Hapo utakutana na Daraja hilo la kustaajabisha.

Tulitaka kujua mawili matatu kuhusiana na daraja hilo,  na hizi ni dondoo ambazo nimekuandalia.

Daraja hili ni la miaka mingi sana tangu enzi za wakoloni (Wamisionary)

Chanzo chake ni kwamba hili ni jiwe kubwa ambalo lilikatiza katika mto Kiwira. Mto ambao hutiririsha maji yake kutoka mlima Rungwe hadi Ziwa Nyasa.

Mwamba huu una tabaka mbili. Yaani mwamba laini na mwamba mgumu.

Kutokana na maji kuwa mengi na kupita juu ya jiwe lile na kudondokea upande wa pili,  basi ikatokea hali ya mwamba laini ambao ulikuwa chini kuliwa hadi kutoboka na hatimaye kutengeneza mfano wa Daraja Gumu na maji kupita chini.

Kutokana na maji kuchimba sana eneo lile limekuwa na kina kirefu sana. 

Kina cha maji yake kinaweza kufikia hadi mita 150.

Juu ya daraja hilo unaweza kuvuka na kutokea upande wa pili wa mto bila tatizo wala masharti yoyote.

Wenyeji wanasema kuwa hapo zamani ilikuwa kama mtu atakuwa na kitu chochote kibaya kama uchawi na kadhalika,  basi asingeweza kuvuka pale. Na hatimaye angedondoka chini na kufa.

Je? Nitaruhusiwa kuoga katika mto huu?

Kwa mgeni haruhusiwi hata kidogo kuoga pale kwa kuhofia usalama wake. Kwani mazingira ni mabovu na maji huenda kwa kasi.

Lakini pia huruhusiwi kuvua samaki katika mto ule.

Ila unaruhusiwa kupiga picha popote upendapo,  kuuliza chochote na hata kunawa maji miguuni au usoni.

Unaweza kuitazama full video hapa chini


Vipi kuhusu maji yake? Yanafaa kwa matumizi?

Maji yake ni safi na unaweza kuyatumia kwa matumizi mbali mbali kama vile kunywa,  kufua nguo,  kuoga n.k.

Sambamba na hilo,  lakini pia muongozaji alituhimiza na kufika sehemu ya juu ya mto ule ambako nayo ina historia yake. Sehemu hii hujulikana kama kijungu.

Hapa kuna maajabu zaidi ya daraja hili la mungu.

Soma: Maajabu ya kijungu huko mto kiwira Tukuyu Mbeya.

Asante kwa kutufuatilia katika makala zetu.

Je? Ulitamani makala ijayo tuzungumzie nini?

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MAMBO USIYOYAFAHAMU KUHUSU DARAJA LA MUNGU MBEYA
MAMBO USIYOYAFAHAMU KUHUSU DARAJA LA MUNGU MBEYA
Vivutio vya watalii ni vingi, huwa tunakusogezea kimoja baada ya kingine. Hili ni Daraja la Mungu Mkoani MBEYA
https://1.bp.blogspot.com/-g0DsP8qyIFE/YD5ljbMZbrI/AAAAAAAAeGU/0rESiV6JMUsAkbbo5rbexk3pvu7WWxIHQCLcBGAsYHQ/s320/images%2B%25283%2529.jpeg
https://1.bp.blogspot.com/-g0DsP8qyIFE/YD5ljbMZbrI/AAAAAAAAeGU/0rESiV6JMUsAkbbo5rbexk3pvu7WWxIHQCLcBGAsYHQ/s72-c/images%2B%25283%2529.jpeg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2021/03/mambo-usiyoyafahamu-kuhusu-daraja-la.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2021/03/mambo-usiyoyafahamu-kuhusu-daraja-la.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content