Kukaa sana chini kuna madhara. Lakini ukidumu na mazoezi haya basi madhara hayo utaendelea kuyasikia kwa wenzako tu tena ambao hawajaisoma makala hii
____________
Mtakie mema mwenzako kwa kumshirikisha makala hii!
____________
Ni mazoezi gani nitafanya ili kuimarisha mwili wangu wakati kutwa nzima nashinda nimekaa?
Jibu ni kwamba;-
Huna haja ya kwenda GYM, Hapo hapo kazini kwako unaweza kufanya mazoezi ambayo yanaweza kuwa msaada mkubwa sana.
Lengo la kuandika mada hii ni kwa ajili ya kunisaidia mimi mwenyewe kwanza kabla ya mtu mwingine. Hii ni kutokana na kazi yangu ya kukaa chini mda mrefu.
Lakini nikaona ili nawe upate manufaa kwa hii post, ni vema nikushirikishe huenda nawe unafanya kazi ambayo inakulazimu ukae mda mrefu katika kiti.
Nawe ambaye umebahatika kusoma makala hii, nakuomba umshirikishe mwingine na mwingine ili aweze kupata madini haya.
Haya hapa ni mazoezi ambayo yatakuwa msaada kwako wewe mwenzangu ambaye karibu mchana wote unashinda umekaa.

1. Nyoosha kiuno
Kukaa chini muda mrefu huathiri maeneo mengi ya mwili, miongoni mwao ni kiuno.
Simama kisha fanya zoezi la kuinama na kusimama mara nyingi. Waweza fanya kadiri ya uwezo wako kuanzia mara 20 na kuendelea kabla hujafanya zoezi jingine.
2. Push ups
Ziko aina nyingi za push ups. Lakini hapa tumekusudia push up zile za kawaida. Weka mikono yako chini kisha nenda kadiri ya uwezo wako kwa mara moja kabla ya kupumzika na kuanza tena.
Utakaposikia misuli inajinyoosha ujue hapo sasa zoezi ndo linafanya kazi.
3. Mazoezi ya Kegel
Kama utakuwa na nafasi unaweza kufanya zoezi hili
Lala chali kisha kita miguu yako na unyanyue sehemu ya kiuno chako kuelekea juu na kurudi chini.
Fanya hivo mara nyingi kati ya 20 na 30 au zaidi.
4. Squat
Hili ni zoezi la kusimama na kuchuchumaa mara nyingi huku mikono yako ukiwa umeshika nyuma ya shingo au umeinyoosha mbele.
Zoezi hili huimarisha zaidi misuli ya magoti, mapaja na miguu kwa ujumla.
5. Tembea kidogo
Kama utakuwa na nafasi, baada ya kukaa kwa muda mrefu unaweza kutembea tembea japo kwa kuzunguka nyumba, uwanja au eneo la karibu yako kabla hujarudi na kuendelea na kazi zako.
Kutoka nje na kutembea husaidia kuimarisha pia akili na kuingiza maarifa mapya. Hii ni kwa sababu kukaa kwa muda mrefu sehemu moja kunadumaza akili na ufahamu.
6. Dead bug
Lala chali kisha nyanyua miguu yako na kuipeleka mbele na kuirudisha mara nyingi.
Pia unaweza kupeleka mguu moja mara kadhaa kisha mguu mwingine.
Nimekuwekea mfano wa picha hapa chini.

COMMENTS