MAKOSA HATARI 8 WANAYOYAFANYA BLOGGERS

Usifanye makosa haya kama unataka kufika mbali

Kila kitu kina miiko yake, kila kitu kina sumu yake. 

Haya hapa chini ni makosa makubwa 8 ambayo hufanywa na waandishi wengi wa blog.

Huenda ukawa hufahamu kama unafanya makosa, au ukachukulia ni kawaida au umeiga sehemu bila kujua kama ni kosa.

Nakuzindua kwa kukuorodheshea hapa chini ili kuweza kuyaepuka haraka iwezekanavyo.

1. Mwandiko mbaya

Hata shuleni mwanafunzi mwenye hati mbaya ya mwandiko, baadhi ya walimu anapomsahihishia daftari lake anaweza wasikague kabisa kile alicho andika.

Mwandiko mbaya ni kero kwa msomaji yeyote yule. Vinginevyo labda kilichoandikwa kiwe ni muhimu sana.

Hivyo jitahidi aina ya muandiko wako iwe ni font ambayo inasomeka vizuri na uwe na rangi nzuri ambayo haiumizi macho.

Soma

Kwanini Blog yako haina watembeleaji?

2. Kuweka kila kitu

Kama unataka kuwa mwana blogg, ni lazima ujue ni kitu gani hasa utajihusisha navyo. Ziko nyanja nyingi na ulimwengu ni mpana. Hivyo angalia upande ambao utaweza na usimame hapo.

Usitake kuweka kila kitu cha duniani kwa kuamini kuwa utawapata watu wengi, si kweli. Mwisho wa siku utawapoteza wasomaji wako.

Vinginevyo labda kama unataka kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Na hapa ni vizuri kuwapa taarifa mashabiki zako ambao wanakufuatilia kila siku.

3. Kutokuwa na mwendelezo

Nadhani unajua kuwa hauko peke yako katika kila unachokifanya, si ndio e?

Mtu atakapoingia katika blog yako na kupendezwa na chapisho lako atasubiri tena muendelezo. Kama akiona kimya hakuna muendelezo anaweza kukukimbia na asirudi teeena.

Mimi mwenyewe kuna watu walikuwa wakiandika vitu vya maana sana lakini kila nikiingia sioni jipya, basi mpaka leo blog zile nimezikimbia.

Kibaya zaidi niliwatafuta mpaka namba zao na sikupata ushirikiano. Sasa fikiria ni wangapi wamekimbia kama mimi?

4. Kutokuzingatia matumizi sahihi ya lugha

Huenda huna taaluma ya uandishi, lakini bila shaka unajua matumizi sahihi ya lugha. Basi zingatia sana hilo.

Kumbuka baadhi ya wasomaji wako ni wajuzi kuliko wewe. Mbali na hilo pia msomaji anakuamini ndio maana leo yupo hapo kwenye blog yako.

Jitahidi sana kuzingatia matumizi sahihi ya lugha, sarufi na sentesi kwa ujumla.

Matumizi ya L na R ni kikwazo kikubwa sana kwa baadhi ya waandishi tena hata wenye taaluma hiyo. Epuka makosa na lugha za matusi.

Vinginevyo labda uwe na sababu ya kufanya hivyo.

Soma

Makosa 10 wanayoyafanya watu wenye youtube channel

5. Kutojifunza

Kubali tu kwamba kila uchao huwa teknolojia inapiga hatua. Hivyo kubaki nyuma kwa kuamini kuwa unaweza ni makosa makubwa ambayo wengi wanayafanya.

Jifunze kutoka kwa wakubwa zako, jifunze kutoka kwa watu mbali mbali wanaofanya kazi mbali mbali.

Kuna ubunifu wa aina tofauti hufanywa na walioendelea. jifunze na kubali makosa pale ambapo umekosea.

6. Blog yako ni rasmi sana

Usiandike kama taarifa ya habari bwana. Usiiweke rasmi kiiiivyo. 

Kumbuka kuwa unatakiwa kuandika kama unazungumza nao na sio kama unawaaagiza au kutoa amri.

Usiandike misamiati ya makusudi ambayo inaweza kuepukika. Usiwafanye watu wasome na kamusi pembeni. Utawaboa

7. Hufanyi utafiti

Usikurupuke:- 


Kama makala unayotaka kuandika hujaifahamu vizuri basi fanya uchunguzi wa kisha ndo uandike.

Kumbuka kuwa kilichoandikwa huishi na kalamu ni hatari kuliko risasi. Kuwa makini katika hilo.

8. Kutojibu comment

Ni faraja sana aliyekutumia maoni yake uyafanyie kazi. Atajiskia kutothaminiwa endapo maoni yake yatakuwa hayafanyiwi kazi kila atumapo.

Kumbuka watembeleaji wako ndio wateja wako na ndio wanao kuweka mjini.

Mthamini msomaji japo kwa kuonesha upendo kwa angalau ku like maoni yake.

Tuandikie maoni yako hapo chini kwa chochote ambacho unahisi ni sahihi kulingana na makala hii.

Naomba nikutakie siku njema

Asante sana kwa kuwa nasi

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MAKOSA HATARI 8 WANAYOYAFANYA BLOGGERS
MAKOSA HATARI 8 WANAYOYAFANYA BLOGGERS
Usifanye makosa haya kama unataka kufika mbali
https://1.bp.blogspot.com/-5nwsLzRHmnE/YI1SK_BjO1I/AAAAAAAAfc4/ylLpQ1bryc44a-yRbWtJHItxy5GIEP6tQCLcBGAsYHQ/s320/mistaces.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-5nwsLzRHmnE/YI1SK_BjO1I/AAAAAAAAfc4/ylLpQ1bryc44a-yRbWtJHItxy5GIEP6tQCLcBGAsYHQ/s72-c/mistaces.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2021/05/makosa-hatari-8-wanayoyafanya-bloggers.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2021/05/makosa-hatari-8-wanayoyafanya-bloggers.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content