UNAWEZA KUFANYA NGONO NA MWENYE UKIMWI NA USIPATE MAAMBUKIZI - KWANINI?

Inawezekana vipi mtu kushiriki ngono na muathirika wa Ukimwi na asipate maambukizi? - Makala hii inakufumbua macho

Inakuwaje unafanya ngono na aliyeathirika na usipate UKIMWI?

Watu wengi wamekuwa na mawazo kuwa ili nipate ukimwi ninatakiwa nishiriki ngono zembe na aliyeathirika mara ngapi? 

Majibu ya swali hili ni mafupi tu, ni kuwa unaweza kuathirika kwa ngono zembe ya siku moja tu ndani ya dakika chache. Lakini jambo la kuzingatia ni kuwa si kila anayeshiriki ngono na aliyeathirika na yeye ataathirika.


Makala hii itakwenda kukufundisha mengi kuhusu somo hili.


Njia ambazo virusi huingia mwilini:-

Kabala ya kuingia ndani zaidi kwenye somo letu, kwanza tujuwe namna ambavyo virusi vya ukimwi vinavyoingia ndani ya miili yetu. Mara tu virusi vinapokutana na mwili wa mtu unaanza kutafuta njia za kuingilia mwilini hadi kufikia kwenye damu. Njia hizo ni kupitia kwenye majeraha, michubuko, matundu yaliyo wazi kwenye vidonda, upele, majibu ama sehemu za mwili zilizo wazi kupitia mikato kama mtu alikatwa na kitu cha ncha kali, ama alichomwa kwa sindano ama kitu cha ncha kali.


Michubuko inaweza kuwa kwenye sehemu za siri yaani uke na uume kutokana na kufanya tendo la ndoa, ama michubuko inaweza kuwa kwenye maeneo mengine ya mwili kutokana na majeraha, mikato ama mikwaruzo. Majeraha na vidonda huweza kupatikana kwenye mdomo ama maeneo mengine ya mwili kutokana na majeraha ama mikato na mikwaruzo. Pia wakati wa kunyoa sehemu za siri huwenda mtu akajikata hivyo kusababisha majeraha madogomadogo.


Nini hutokea baada ya virusi kuipata njia ya kuingia mwilini?

Kitu cha kwanza virusi huhitaji kuingia kwenye damu. Vinapofika kwenye damu vinatafuta seli zinazofahamika kwa jina la CD4. Katika damu aina zisizopunguwatatu za seli. Kuna seli hai nyekundu za damu, kuna seli hai nyeupe za damu na pia kuna seli sahani. Seli hai nyekundu kazi yake kuu ni kusafirisha hewa ya oksijeni kwenda maeneo mengine ya mwili. Kazi kuu ya seli hai nyeupe ni kulinda mwili na kukinga dhidi ya vijidudu vya maradhi kwa kuviuwa vijidudu hivi.

Sasa virusi vya ukimwi vinapoingia kwenye damu moja kwa moja hutafuta seli hai nyeupe inayofahamika kwa jina la CD4 na kuingia ndani. Lengo lake ni kwenda kuzaliana humo. Hivyo virusi vinapoingia kwenye seli hizi vinaanza kuzaliana na vikijaa kwenye seli hupasuka na kumwaga maelfu ya virusi kwenye damu, kisha mchakato huendelea kwenye seli nyingine. 

Kwa njia hii virusi vinajaa mwilini na kuathiri seli nyingi zaidi na kila seli inapojaa virusi hupasuka na kufa. Kadiri seli zinapokufa ndipo kinga ya mwili hupunguwa na hatimaye kupata upungufu wa kinga mwilini.


Sasa inakuwaje inakuwaje mtu anashiriki tendo la ndoa na mtu aliyeathirikabila ya kuathirika?

Ok, sasa turudi kwenye swali letu la msingi. Bila shaka umejifunza hapo juu njia ambazo virusi huingia mwilini. Wapo watu wengi walioishi miaka kadhaa na waathirika bila ya wao kuathirika na hali wanazaa watoto na hata hawatumii kinga. Unadhani ni kitu gani hapa hutokea. 


Zifuatazo ni baadhi tu ya sababu:-

a) Kama wameshiriki ngono kwa kutumia kinga kifasaha na kujilinda na hatari zinazoweza kutokea wakati wa tendo kama kupasuka kwa kondom. Kama wamechukuwa thadhari vyema hawawezi kuambukizana.

b) Kama hakuna michubuko yeyote iliyotokea wakati wa tendo.

Maambukizi ya VVU kupitia ngono mara nyingi hutokea kama kumetokea michubuko kwenye sehemu za siri uume ama uke wakati wa tendo. Michubuko hii ni midogo kiasi kwambu unaweza usihisi chochote. Sasa kama tendo lilifanyika kistarabu, kiupole na kwa utaratibu mzuri ni vigumu kutokea kwa michubuko hivyo si rahisi mtu kuathirika hata kama alishiriki na muathirika.

c) Kama muathirika alikuwa ni mtumiaji wa dozi ya ARV kwa ufasaha kwa mda mrefu hata akafikia idadi ya virusi kwenye kipimo cha damu ni 0, akifikia hatuwa hii hawezi kumuambukiza mtu mwingine hata kama hawakutumia kinga.


Je nawezaje kuzuia kutopata michubuko wakati wa tendola ndoa?

Hili ni swali zuri, ila kabla ya kulijuwa uzuri wa swali hili, nakupa swali jingine. Je kuna umuhimu gani wa kujizuia kutopata michubuko wakati wa tendo la ndoa? Kwa ufupi wa majawabu ni kuwa, michubuko ndio njia ambazo virusi huweza kuingia mwilii, sasa kama hatuna michubuko si rahisi kwa virusi kuingia mwilini. 

Sasa wacha tuone njia ambazo unaweza kutumia kuzuia michubuko wakati wa tendo:-


1. Kwa kutumia vilainishi. 

Vilainishi hivi vinaweza kuwa mafuta ama vilainishi vingine vya asili. Kawaida mwili wa mwanamke una vilainishi ambavyo hupunguza msuguano na kuzuia michubuko ila si kila wakati vilainishi hivi vitakuwepo kwa muda wote.

  

2. Kuandaa mwili wa mwanamke hata kabla ya kuanza kwa tendo.

 Maandalizi haya ni muhimu katika kuhakikisha kuwa mwili wa mwanamke unatowa majimaji ambayo ndio vilainishi vya asili.


3. Tendo lifanyike kwa upole na kwa ustaarabu na kwa hisia.

 Endapo hisia za mwanamke zitakata ni vyema kustop hadi zirudi ili kuwepo kwa majimaji, kwani endapo zitakata hatoweza kuwa na majimaji ambayo ndio vilainishi vya asili vinginevyo mafuta yatumike kama vilainishi mbadala.

Tendo lisifanyike kwa muda mrefu sana, kawaida kama tendo litafanyika kwa muda mrefu ni vigumu kwa mwili wa mwanamke kuendelea kuzalisha vilainishi muda wote, hivyo uwezekano wa kupata michubuko ni mkubwa sana.


Inakuwaje idadi ya virusi ikawa 0 kwenye damu na mtu akawa ni muathirika?

Vipimo vya virusi vya ukimwi vipo vya aina nyingi. Kuna ambavyo hupima idadi ya virusi kwenye damu na kuna ambavyo hupima antibody zinazotolewa na virusi. Kitaalamu idadi ya virusi kwenye damu hufahamika kama viral load. Sasa hutokea wakati kwa yule anayetumia dawa za VVU ikafikia idadi ya virusi kwenye damu yake inawa ni sifuri. 

Hii hutokea kama ametumia dawa kwa muda mrefu usiopunguwa miezi 6, na akawa anafuata masharti yote. Sasa endapo atadumu na hali hii kwa muda wa miezi 6 hawezi kumuambukiza mtu. 

Sasa lamda tuone hali hii inatokeaje. Kawaida kama mtu ameanza mapema kutumia ARV basi dawa hizi huzuia uzalishaji wa virusi hivi ama hupunguza visizaliane ama hupunguza visisathiri seli nyingine. Kama mtu atatumia vema dawa virusi vinakwenda kujificha maeneo mengine ya mwili na vinaondoka kwenye damu, na hapa ndipo hufikia mtu anawa hana kabisa virusi kwenye damu.

Sasa kwa kuwa virusi hivi bado vipo mwilini ila vimejificha tuu, vitaendelea kuzalisha kemikali zinazofahamika kama antibody, kemikali hizi ndizo hutuonyehsa kuwa bado vipo mwilini ila vimejificha. Endao mtu ataacha kutumia dawa vitarudi tena kwa kasi kubwa na kwa nguvu mpya na kuathiri mwili kwa haraka Zaidi. Ikifikia hali hii mtu huambiwa kitaalamu ana viral resistance yaani virusi vyeke vimetengeneza usugu.

Tukutane Makala ijayo tutakapozungumzia watu walio hatarini kupata maambukizi na dawa wanazopaswa kutumia kama tahadhari kwao.

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: UNAWEZA KUFANYA NGONO NA MWENYE UKIMWI NA USIPATE MAAMBUKIZI - KWANINI?
UNAWEZA KUFANYA NGONO NA MWENYE UKIMWI NA USIPATE MAAMBUKIZI - KWANINI?
Inawezekana vipi mtu kushiriki ngono na muathirika wa Ukimwi na asipate maambukizi? - Makala hii inakufumbua macho
https://1.bp.blogspot.com/-TMNPo6xB4qM/YM2ZUd1do8I/AAAAAAAAhrg/ty9Ycf4qlQgx45F1wRoAm8iuo1nDqKpZwCLcBGAsYHQ/s0/AWc7p5wwR2ErHyRCd7dk.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-TMNPo6xB4qM/YM2ZUd1do8I/AAAAAAAAhrg/ty9Ycf4qlQgx45F1wRoAm8iuo1nDqKpZwCLcBGAsYHQ/s72-c/AWc7p5wwR2ErHyRCd7dk.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2021/06/unaweza-kufanya-ngono-na-mwenye-ukimwi.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2021/06/unaweza-kufanya-ngono-na-mwenye-ukimwi.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content