VIDONDA VYA TUMBO - CHANZO, DALILI NA TIBA ZAKE

Eti vidonda vya tumbo HAVITIBIKI? - Si kweli. Soma makala hii ili kupata faida zaidi

Vidonda vya tumbo ni katika matatizo ya kiafya ambayo yamekuwa yakiathiri watu wengi leo. 

Si wanawake tu lakini hata wanaume, wazee kwa watoto. Kumekuwa na fikra nyingi potofu kuhusu vidonda vya tumbo nini hasa sababu zake, dalili zake na kwa namna gani vidonda vya tumbo hutokea. 

Je na wewe ni katika watu hawa?. makala hii ni kwa ajili yako. Lengo la makala hii ni kukujuza dalili za vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo ni vidonda ambavyo hutokea kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Vinaweza kutokea kuanzia eneo la juu la tumbo la chakula, kuelekea kwenye tumbo, utumbo mdogo hadi utumbo mkubwa. 

Vidonda hivi pia vinaweza kuathiri koo la chakula. Mara nyingi watu wamekuwa wakidhani vidonda vya tumbo vipo kwenye tumbo la chakula tu. Hii sio sahihi kabisa. 


Labda tuone aina za vidonda vya tumbo

Vidonda vya tumbo vimegawanyika katika aina zisizopunguwa tatu. Miongoni mwazo ni 

a) Vidonda vya tumbo vinavyotokea kwenye tumbo la chakula, 

b) Vidonda vya tumbo vinavyotokea kwenye sehemu inayounganisha koo la chakula na tumbo la chakula 

c) Vidonda vya tumbo vinavyotokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo.


Nini chanzo cha vidonda vya tumbo?

Watu wengi wamekuwa wakidhania kuwa chanzo cha vidonda vya tumbo ni kukaa na njaa muda mrefu. 

Kwa namna moja wapo sahihi. Lakni ukweli ni kuwa hiki sio chanzo kikuu. Na wanaopata vidonda vya tumbo kwa sababu hii ni wachache sana. 

Chanzo kikuu cha vidonda vya tumbo ni mashambulizi ya bakteria wanaojulikana kama Helicobacter pylori (H.pylori) hawa ni bakteria ambao wanakwenda kushambullia tumbo na utumbo hatimaye kusababisha vidonda.

Vyanzo vingine vya vidonda vya tumbo ni kama matumizi ya aina flani za dawa kwa muda mrefu. Mfano mzuri ni dawa za kutuliza maumivu zinazofahamika kama NSAIDs kirefu chake ni  'Nonesteroidal anti-inflamatory drugs' mfano wa dawa hizi ni kama advil na aleve. 

Chanzo kingine cha vidonda ni misongo ya mawazo kwa muda mrefu, na chanzo kingine ni uzalishwaji wa tindikali kuongezeka ndani ya mwili.

Je ni kivipi vidonda hutokea?

Kwa ufupi vidonda hutokea baada ya utando mlaini kwenye tumbo na utumbo kulika na kubakisha tumbo ama utumbo kuwa wazi hivyo kuruhusu shughuli za tindikali kuathiri tumb na utumbo.

 Hii husababisha michubuko na hatimaye kuleta vidonda vya tumbo. Bila shaka huwenda hujaelewa hapa. Wacha nikujuze zaidi.

Soma pia;-

Mazoezi 6 yanayoongeza nguvu za kiume

Katika tumbo na utumbo kuna tindikali (acid) ambazo huzalishwa mwilini kwa ajili ya kuuwa bakteria kwenye vyakula. Zipo kazi nyingine pia. 

Tindikali hizi zina nguvu kiasi hata kuraruwa bati. Sasa kwa nguvu hii hata ngozi inaweza kuchubuka na kusababisha vidonda. Sasa kwa kuwa kwenye tumbo na utumbo kuna utando wa utelezi huu husaidia kuzuia athari ya bakteria haiathiri utumbo na tumbo.

Hivyo basi, endapo utando huu utaathirika na hautakuwepo tena ama utakuwepo kwa uchache hali hii itaruhusu tindikali zinazozalishwa kwenye tumbo na utumbo kuchubuwa kuta za utumbo na utumbo na hatimaye kusababisha vidonda. 

Kuhusu bakteria wanavyosababisha vidonda inaweza kuwa tofauti kidogo. 

Wao bakteria kwanza mara nyingi hawana shida wanaweza kuishi mika mingi bila ya kusababisha vidonda. Sasa wakati mwingine wanaweza kusababisha kuta laini za utumbo na tumbo kuvimba. Hii mivimbo baadaye kusababisha vidonda.

Hutokea pia tindikali zikaunguza utando laini huu unaokinga ngozi ya tumbo na utumbo. Hii hutokea endapo uzalishwaji wa tindikali utaongezeka. Hii inaweza kusababishwa na vyakula, misongo ya mawazo ama matumizi ya dawa kama ilivyoelezwa hapo juu.


Ni zipi dalili za vidonda vya tumbo?

Dalili za vidonda vya tumbo zinaweza kuwa tofauti kutokana na mtu mwenyewe, mahali vilipo na mengineyo lakini zipo ambazo hutokea kwa watu karibia wote. 

Dalili hizo ni kama:-

- Tumbo kujaa gesi

- Kiungulia cha mara kwa mara

- Maumivu ya tumbo hasa unapokuwa na njaa

- Uchovu wa mra kwa mara

- Kupata choo cheusi ama chenye damu

- Huwenda ukatapika damu

- Inaweza tokea ukapunguwa uzito

- Kukosa hamu ya kula


Mgonjwa anaweza kupata nafuu ya maumivu baada ya kula na kushiba. Pia kuna wengine wanapata nafuu baada ya kunywa maziwa. Lakini tambuwa kuwa ijapokuwa maziwa yanaweza kukupa nafuu lakini sio mazuri huwenda yakaja kukuletea madhara huko siku za mbele.


Je vidonda vya tumbo vinatibika?

Jibu fupi ni 'NDIO', Vidonda vya tumbo hutibika tena bila ya ugumu wowote. 

Vindonda vya tumbo vinaweza kutibika kwa dawa za asili kama bamia, kabichi, kitunguu thaumu, asali na nyinginezo. Lakini pia ni vyema kutumia dawa za hospitali kwa sababu zina vipimo maalumu.

Soma pia

Siri 6 usizozifahamu zinazopatikana kwa kula bamia

Vidonda vya tumbo vinaweza kuwa sugu. Na hii hutokea endapo utumiaji wa dozi hautafata masharti. 

Lakini pia inawez akutokea bila ya sababu maalumu. Wakati mwingine vidonda vya tumbo huwa sugu kwa sababu tiba yake sio inayotumika. Ili kuweza kutokomeza vidonda vya tumbo kwanza ni kujuwa sababu gani inayosababisha vidonda vya tumbo.

Kama sababu ni tindikali kuzaliwa nyingi basi mgonjwa apewe dawa za kuzuia uzalishwaji wa tindikali kutokuwa mwingi zaidi. Na kama sababu ni matumizi ya dawa mgonjwa aangaliwe kama ataweza kubadilishiwa dawa. Na kama sababu ni bakteria mgonjwa atapewa dawa ya kuuwa bakteria hao tumboni.


Imani potofu kuhusu vodona vya tumbo

Kama nilivyokueleza mwanzoni mwa makala hii kuwa kuna imani nyingi potofu na hazina ushahidi wa kitaalamu. Inaweza kuwa watu ndivyo wanavuyoamini kutokana na jamii zao ama kutokana na tafiti za zamani ambazo kwa sasa zimekosolewa kutokanana tafiti mpya.

 Imani hizo ni kama:-

Vyakula vyenye pilipili husababisha vidonda vya tumbo. Hii si kweli

Kukaa na njaa ndio sababu kubwa ya kutokea vidonda vya tumbo. hii si kweli

Vidonda vya tumbo havitibiki, hii ia si kweli.

Tukutane makala ijayo tutakapoona vyakula vizuri na vibaya kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: VIDONDA VYA TUMBO - CHANZO, DALILI NA TIBA ZAKE
VIDONDA VYA TUMBO - CHANZO, DALILI NA TIBA ZAKE
Eti vidonda vya tumbo HAVITIBIKI? - Si kweli. Soma makala hii ili kupata faida zaidi
https://1.bp.blogspot.com/-Oc3qTp37X-Q/YMC1tnH-I_I/AAAAAAAAhM4/1L8ZkjVsBucW9UsgcpTG6wQdditzTKawQCLcBGAsYHQ/s320/1800x1200_visual_guide_to_stomach_ulcers_slideshow.webp
https://1.bp.blogspot.com/-Oc3qTp37X-Q/YMC1tnH-I_I/AAAAAAAAhM4/1L8ZkjVsBucW9UsgcpTG6wQdditzTKawQCLcBGAsYHQ/s72-c/1800x1200_visual_guide_to_stomach_ulcers_slideshow.webp
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2021/06/vidonda-vya-tumbo-chanzo-dalili-na-tiba.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2021/06/vidonda-vya-tumbo-chanzo-dalili-na-tiba.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content