VYAKULA HATARI KWA MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO

VYAKULA VYA KUVIEPUKA KWA MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMB

Vidonda vya tumbo ni nini?

Vidonda vya tumbo ni aina za vidonda ambavyo hutokea kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. 

Vidonda hivi vinaweza kutokea kwenye tumbo ama utumbo. 

Hata hivyo koo la chakula linaweza kuathirika kupata vidonda, jambo hatuviiti vidonda vya tumbo. 

Vidonda vya tumbo vinaweza kuleta maumivu makali sana ya tumbo na mara nyingi hutokea wakati mtu ana njaa.

Nini husababisha vidonda vya tumbo?

Sababu kuu ya kutokea kwa vidonda vya tumbo ni mashambulizi ya bakteria wanaojulikana kama Helicobacter pylor (H.pylor). bakteria hawa wanaishi kwenye tumbo. 

Mtu anaweza kuishi na bakteria hawa kwa miaka mingi bila ya kusabbabisha madhara yeyote yale. 

Lakini si mara zote, bakteria hawa wanaweza kusababisha kuvimba (inflamation) kwenye kuta za tumbo, na kupelekea kutokea kwa michubuko na hatimaye vidonda vya tumbo. 

Vingine vinavyosababisha vidonda vya tumbo ni kama:-

- Misongo ya mawazo

- Ongezeko la uzalishwaji wa tindikali tumboni

- Matumizi mabaya ya dawa

- Saratani ya tumbo

Dalili za vidonda vya tumbo

Maumivu ya vidonda vya tumbo ni makali, pia mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kupatwa na changamoto nyingine ambazo ni katika dalili za vidonda vya tumbo. 

Kwa mfano kutapika, kiungulia cha mara kwa mara, tumbo kujaa gesi, maumivu ya kifua, kupungua kwa damu na uzito.

 Endapo vidonda vya tumbo vitadumu kwa muda mrefu bila ya kupatiwa matibabu afya ya mgonjwa inaweza kuwa mbaya ijapokuwa vidonda vya tumbo havisababishi kifo.

Vipi nitatuliza maumivu?

Unaweza kutuliza maumivu ya vidonda vya tumbo kwa kutumia dawa za hospitali. Pia kwa kutumia dawa za kienyeji. 

Lakini unaweza kutuliza maumivu haya kwa kutumia vyakula. Wapo baadhi ya wagonjwa wa vidonda vya tumbo hutumia baadhi ya vyakula kutuliza maumivu. Mfano wa vyakula hivyo ni maziwa.

Tulisha eleza kwa kina kuhusiana na vidonda vya tumbo, chanzo na dalili zake. Soma makala hii hapa chini

Chanzo na Dalili xa vidonda vya tumbo

Endelea na makala hii hapo chini utajifunza vyakula hivi vilivyo vizuri kwa vidonda vya tumbo.

Nini husabaabisha maumivu?

Maumivu ya vidonda vya tumbo pia yanaweza kusababishwa na matumizi ya madawa na vyakula ama vinywaji fulani. 

Pia kukaa na njaa kwa muda mrefu kunaweza kuleta maumivu kwa mgonjwa. Hutokea pia misongo ya mawazo ikawa pia ni vichochezi vya maumivu haya. 

Huenda mgonjwa anatumia hivi bila ya yeye kujua ama anatumia kwa sababu hana namna nyingine ya kufanya. 

Kwa mfano ijapokuwa maziwa hutuliza maumivu lakini kitaalamu sio mazuri sana kwa mgonjwa. 

Endelea na makala hii hapo chini utajifunza vyakula hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo;-

Vyakula anavyopasa kula mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Ni ngumu sana hapa kuanza kukuorodheshea orodha ya vyakula vyote anavyotakiwa kula mgonjwa wa vidonda vya tumbo. 

Hata hivyo kila jamii ina aina ya vyakula vyao ambavyo ni ngumu kujulikana kwa watu wa jamii nyingine. 

Hapa nitakuletea tu kanuni ambazo utaziangatia pindi unapochaguwa chakula kwa ajili ya kutumiwa na mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Angalia vyakula vyenye sifa hizi:-

- Vyakula ambavyo havina gesi 

- Vyakula ambavyo havina uchachu sana

- Vyakula ambavyo havina chumvi nyingi sana

- Vyakula ambavyo havina mafuta mengi

Pia vyema ukatumia na vyakula vifuatavyo kwa namna ambayo unaona itafaa kwa upande wako:-

- Kabichi

- Matunda aina ya ma epo

- Karoti

- Mboga za majani za kijani

- Asali

- Kitunguu thaumu


Vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo:


*********************
Kama nilivyokueleza hapo juu kuhusu kanuni za kuzishikilia unapochaguwa vyakula basi hapa pia utaendelea na kanuni zile zile pindi unapotaka kuepuka vyakula ukiwa kama mgonjwa wa vidonda vya tumbo. 

Epuka vyakula hivi:-

- Vyenye gesi kama maharagwe

- Vyenye uchachu sana (Kama ndimu n.k)

- Vyenye pilipili kwa wingi

- Vyenye mafuta mengi

- Vyenye chumvi nyingi


Pia punguza matumizi ya vifuatavyo ama wacha kabisa iwezekanapo:-

- Sigara

- Pombe

- Kahawa

- Maziwa unaweza kupunguza tu matumizi

- Pilipili kwa wingi


Vipi nitajilinda na vidonda vya tumbo?

Ni ngumu sana kwa sababu mpaka leo bado haijajulikana sababu ya kupata bakteria wa vidonda vya tumbo. 

Hivyo kujikinga na vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na mashambulizi ya bakteria ni ngumu. 

Ila kwa kuwa sababu za kutokea kwa vidonda vya tumbo ni nyingi, unaweza kujikinga na vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na sababu nyingine. 


Njia hizo ni kama:-

- Punguza misongo ya mawazo

- Wacha ama punguza kutumia kilevi

- Punguza ama wacha kabisa kuvuta sigara

- Wacha kutumia dawa kiholela

- Je vidonda vya tumbo vinaweza kupona kabisa?

Tambuwa kuwa vidonda vya tumbo vinatibika bila ya wasi wowote ule. Unaweza kutibiwa na ukapona kabisa. 

Hakuna muda maalumu wa kupona lakini haiwezi kumaliza miezi hata sita utapona kabisa. 

Tukutane makala inayofata takapojifunza kuhusu matibabu na dawa za vidonda vya tumbo.

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: VYAKULA HATARI KWA MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO
VYAKULA HATARI KWA MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO
VYAKULA VYA KUVIEPUKA KWA MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMB
https://1.bp.blogspot.com/-fDdMgtn0VQI/YMcGc7wmkEI/AAAAAAAAhow/dhjpXvoebQwKn6wdOKlLzTCjEuNj3sSIACLcBGAsYHQ/s320/OyEs4jzjlPFruits.jpeg
https://1.bp.blogspot.com/-fDdMgtn0VQI/YMcGc7wmkEI/AAAAAAAAhow/dhjpXvoebQwKn6wdOKlLzTCjEuNj3sSIACLcBGAsYHQ/s72-c/OyEs4jzjlPFruits.jpeg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2021/06/vyakula-hatari-kwa-mgonjwa-wa-vidonda.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2021/06/vyakula-hatari-kwa-mgonjwa-wa-vidonda.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content