MATIBABU SAHIHI, DAWA 8 NZURI ZA MINYOO

Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa utajifunza mengi kuhusu aina za minyoo na matibabu yako.

______________
Minyoo ni katika aina ya parasites ambao huingia ndani ya miili na humo huishi na kujipatia chakula chao katika mwili wa mtu waliomuingia.

Kuna aina nyingi za minyoo lakini wapo kadhaa tu ndio huweza kuwaathiri wanadamu kwa mfano minyoo wanaojulikana kama thread worm.

Dawa zinazotumika kutibu minyoo hujulikana kama anthelmitics. Mfano wa dawa hizi ni mebendazole. Je unajuwa dawa nyingine za minyoo na aina za minyoo.

Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa utajifunza mengi kuhusu aina za minyoo na matibabu yako.


Ni zipi aina za minyoo?

Minyoo pia huitwa helminth wapo katika aina nyingi sana. Lakini si minyoo wote wanaweza kuingia kwenye mwili na kusababisha madhara. Minyoo wanaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu ambayo ni:-


 1. Minyoo aina ya roundworm:- Mfano ya minyoo wanaopatikana kwenye kundi hili ni threadworm, ascaris, hookworms and trichuris. Tunaweza kuwapata minyoo hawa kwa kula mayai yao kupitia maji ama vyakula. Ndani ya miili yetu minyoo hawa wanaishi kwenye utumbo mdogo. Humo ndipo ambapo mayai yao hutotolewa na kuwa na viminyoo vipya ambavyo baadaye hutaga na kuwa na minyoo mingi zaidi.


Pata na Faida hii👇

                                             

 1. Minyoo aina ya tapeworm:- Hawa wana vipingili kama vile tandu laini ni warefu kama ile anayopimia fundi cherahani kama wanavyoonekana kwenye picha. Hawa tunaweza kuwapata kwa kula vyakula ambavyo havijaiva vyema ama havijapikwa kabisa. Ulaji wa matunda bila ya kuosha huchangia kupata minyoo hawa. Nyama ambayo haijawiva vyema inaweza kuwa chanzo cha kupata minyoo hawa. Ndani ya miili yetu minyoo hawa huishi kwenye tumbo.


 1. Minyoo aina ya flukeworm:- Hawa ni minyoo ambao ni hatari sana. Wanaweza kluishi kwenye maeneo engi ya mwili na yaliyo hatari. Pia athari yao kiafya ni kubwa. Kwa mfano wanaweza kuishi kwenye mishhipa ya damu, kwenye mapafu na kwenye ini. Na wanapoishi humo hula kiungo husika. Kama unakumbuka kichocho ni moja ya ugonjwa unaosababishwa na minyoo hawa. Unaweza kuwapata kwa kuogelea kwenye maji yenye minyoo hawa.


Je ni yapi matibabu ya minyoo?


Kuna aina ya dawa nyingi sana ambazo hutumika kutibu minyoo. Dawa aina ya mebendazole ni katika dawa za minyoo zilizo maarufu sana. Karibia matuka yote ya dawa utaipata. Na hii ni kwa sababu hutibu minyoo ambayo ndio watu wengi wanayo. Dawa nyingine za kutibu minyoo ni kama:-

 1. Levamisole

 2. Niclosamide

 3. Prazziquantel

 4. Albendazole

 5. Diethylcarbamazine

 6. Ivermectin

 7. TiabendazoleNi nini husababisha kupata minyoo?

 1. Kunywa maji yasio salama na safi kunaweza kufanya ukanywa na mayai ya minyoo. Ni vyema kuchemsha maji kama upo meneo yenye maji machafu

 2. Kula udongo ambao una mazalia ya minyoo. Kwa wale walaji udongo wawe makini sana ni rahisi kupata minyoo.

 3. Kugusa kinyesi kisha mayai ya minyoo ukayapata. Kwa bahati mbaya yanaweza kufika mkononi na ukayala

 4. Hali ya usafi kuwa mbaya kuanzia mazingira na mwili

 5. Kuwa na tabia ya uchafu, unakula bila ya kuosha ama kunawa.


Nini hutokea kama minyoo haitatibiwa mapema?

 1. Kuendelea kwa dalili za minyoo kama kukosa hamu ya kula, njaa mara kwa mara ukila kidogo huna hamu, maumivu ya tumbo, uchofu na nyinginezo

 2. Minyoo inaweza kusababisha upungufu wa damu

 3. Kupunguwa uzito.

 4. Miwash ya ngozi.


Je minnyoo inasababisha vidonda vya tumbo?

Si kawaida kwa minyoo kusababisha vidonda vya tumbo. Kwani sababu kuu ya vidonda vya tumbo ni mashambulizi ya bakteria aina ya H.pylori. Kuna tafiti zinaonyesha kuwa aina ya minyoo wanaoishi kwenye utumbo mdogo wanaofahamika kama Intestinal Fluke wanaweza kusababisha vidonda kwenye utumbo mdogo.


Soma pia

Matibabu sahihi ya vidonda vya tumbo


Ni kitugani hasa minyoo inakula katika miili yetu?

Pindi tu minyoo inapoingia ndani ya miili yetu inakuwa imepata nyumba. Humo itazaliana na kuishi na kula na hupata hewa humo. Minyoo ndani ya mwili wa mnyama ama binadamu inaweza kula:-

 1. Inakunywa damu

 2. Inakula chakula unachokula

 3. Inakula virutubisho

 4. Inaweza kula viungo vingine kama ini.


Unaweza kujikinga na minyoo kwa kuwa msafi wa mwili, mazingira, vyakula, vinywaji na vyakula vipikwe vyema.


Tukutane makala ijayo tutaangalia kwa udani vyanzo vya minyoo, na kwa namna gani minyoo huingia mwilini mwetu na wapi hukaa pindi inapoingia.


Pia tutaona athari zake na vyakula vikuu vyenye mivyoo kwa wingi.


_______________

Mwandishi wa Makala

DR Rajabu Athumani kutoka bongoclass.com


Mhariri - SAIDI BUNDUKI Kutoka mrbunduki.com

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MATIBABU SAHIHI, DAWA 8 NZURI ZA MINYOO
MATIBABU SAHIHI, DAWA 8 NZURI ZA MINYOO
Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa utajifunza mengi kuhusu aina za minyoo na matibabu yako.
https://1.bp.blogspot.com/-NErA00bqxUg/YPBb7a3VoUI/AAAAAAAAhxQ/s4eaF7lOpZUSAj4lB6qO0wH-cqnL16sSwCLcBGAsYHQ/w371-h172/DAWA%2BZA%2BMINYOO.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-NErA00bqxUg/YPBb7a3VoUI/AAAAAAAAhxQ/s4eaF7lOpZUSAj4lB6qO0wH-cqnL16sSwCLcBGAsYHQ/s72-w371-c-h172/DAWA%2BZA%2BMINYOO.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2021/07/matibabu-na-dawa-za-minyoo.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2021/07/matibabu-na-dawa-za-minyoo.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content