TATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI NA SULUHISHO LAKE

Pa pa pa, ndani ya sekunde 30 - dakika 1 mzee ushamaliza. Unaiona dunia yote imekuelemea na hujui cha kufanya. MAKALA HII NI MSAADA KWAKO

Kama kuna mtiririko wa matukio yanayowasumbua wanaume katika mapenzi basi na hili ni mojawapo. Baadhi ya wanaume hasa vijana wamekuwa wakilalamikia tatizo hili na kupata taabu na mashaka katika mahusiano / ndoa zao.

Kuwahi kufila kileleni ni kupi?
Hii ni hali ya kuwahi kumaliza tendo kabla ya muda wa kawaida. Kwa mwanaume mwenye afya njema kwa mzunguko wa kwanza angalau atumiekuanzia dakika 6 hadi 9 tangu kuanza tendo (Sio utangulizi)

Kama unaenda chini ya dakika 2 hapo tunaweza kusema kuwa umewahi kufika kileleni.

Lakini dharura zipo, huenda ni siku moja moja. Kukosea na kufeli kwa mwanaume kupo. Ila tunachokitafutia njia hapa ni yule ambaye kila siku anaangusha gari.

__________

Nimeamua kukupa njia na tiba ya kumaliza tatizo hili la fedheha hasa kwa kijana. Lakini kabla ya kuangalia njia za matibabu na suluhisho tuangalie kwanza vyanzo vya tatizo.

‘Kama unapenda kujifunza kuhusu utalii wa ndani basi nikukaribishe kuitembelea channel yetu ya BUNDUKI TV ambayo ni sehemu pekee itakayokujuza mengi na kukata kiu yako. BOFYAHAPA’


Sababu za kuwahi kufika kileleni (mwanaume)

 Ziko sababu za kibaiolojia na za kisaikolojia. Ila nitakuambia zote kwa pamoja.


Sababu za asili / kurithi

Hizi ni sababu za kuzaliwa, ni aina ya watu ambaye amezaliwa na tatizo hili au amerithi kutoka kwa wazazi wake. Kwa tatizo hili ni vema kumuona daktari wa masuala ya afya ya uzazi kwa maelekezo zaidi.


Kutarajia kufeli

Wengine hutawaliwa na hofu kabla ya tendo kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo huenda alishawahi kufeli siku za nyuma kabla.

Ugeni kwa mwanamke husika na mazingiza vinaweza kuchangia kuongeza hofu.


Kujichua (Punyeto)

Tulishaelezea kwa kina kuhusiana na madhara ya kupiga punyeto. Na hii ni miongoni mwa madhara yake makubwa, unajua ni kwanini?

Kwa sababu kujichua mtu huwa anajikadiria mwenyewe na pia mkono hauna joto kama ilivyo kwa mwanadamu. Hivyo anapokuwa na mpenzi ni ngumu kuweza kujizuia kufika kileleni kwa haraka kutokana na kuzoea mkono wake.


Papara uwanjani

Mwanamke umemfukuzia kwa muda mrefu bila mafanikio, siku unampata unakuwa unawaza moja kwa moja penzi lake na hatimaye ndani ya dakika moja unakuwa umeshamaliza au hata kabla ya kuanza (kwa baadhi yao).


Kukaa muda mrefu bila kufanya mapenzi

Hii inatokana na kujaa kwa kibubu cha manii (shahawa). Siku ukikutana na mwanamke inakuwa sio rahisi kutumia hata dakika 3. Inamaana chini ya dakika mbili unakuwa umeshajimaliza.

Hili linakuwa sio tatizo sana kama utaweza kuendelea na kudumu na tendo.


Staili ya mapenzi

Kuna baadhi ya staili ambazo humchochea sana mwanaume kuwahi kumaliza kutokana na staili hizo kuwa na msisimko wa hali ya juu. Ziepuke katika raundi ya kwanza.

Sina haja ya kuzitaja hapa.


Msongo wa mawazo

Maisha yanatuadhibu katika njia mbali mbali. Kiasi ambacho hupelekea kuathiri hata mahusiano yetu na wenzetu.

Epuka sana kukaribisha mawazo potofu wakati wa tendo, mwisho wa siku unaweza ukawa kama sanamu lakini akili haipo mahala hapo na kujikuta unamaliza bila hata kujielewa na kutomtendea haki mwenzi wako.


Kuangalia picha za ngono (porn)

Kuna wanandoa huwa na utaratibu wa kuangalia picha za ngono aidha wakiwa pamoja au mtu akiwa peke yake.

Hii hatari yake ni kwamba unaweza kumuwaza mtu uliyemuona katika picha na akakuvutia kuliko mwenzi wako. Hatimaye wakati wa kufanya mapenzi ukajikuta unawaza maumbile na utundu uliouona kwenye video ya ngono na hatimaye unamaliza kabla ya muda wa mweza kuridhika.

 

SULUHISHO

 • Fanya mazoezi
 • Muandae mwanamke kabla ya kumuingilia
 • Usiwaze sana tendo wakati unafanya
 • Jifunze kurudisha mkojo

Fanya mazoezi ya kubana mkojo wakati unakwenda kukojoa mkojo wa kawaida. Ubane kwa sekunde kadhaa kisha uachie. Fanya hivyo kila unapokwenda haja ndogo. Utazoea na utaweza kubana manii wakati wa kungonoka.

 • Wacha punyeto
 • Punguza kula vyakula vinavyoongeza hisia
 • Kama umeoa usikae muda mrefu bila kufanya
 • Epuka / Acha kuangalia ngono
 • Kula chakula bora na matunda
 • Zungumza na mwenzako
 • Usianze na staili tata kwako
 • Fika hospitali / waone wataalamu wa afya ya uzazi.

 

Madhara ya mwanaume kuwahi kufika kileleni

Kudharaulika

Jamani dharau ni mbaya asikwambie mtu. Hasa kudharauliwa na mtoto wa kike kwa sababu umeshindwa kumridhisha.. Daaah acha tu. Na hiyo inapelekea sababu namba mbili hapa chini.


Mwanamke kuchepuka

Kama unadumu kwa muda mrefu na mwanamke bila kumridhisha unatarajia nini kitatokea? Ukizingatia wanawake wenyewe wameshapita sehemu mbali mbali kwahiyo wanajua mwanaume kamili  anakuwaje na mwanaume mgonjwa nakuwaje. Hapo tarajia kukimbiwa ndugu yangu.

Kibaya zaidi ni kupelekea sababu namba tatu hapo chini hutokea.


Stress

Mbali na stress zako za kukosa pesa, hatimaye unaongezewa stress za mapenzi kwa kuona mwanamke wako ana mwanaume mwengine kama sio kukukimbia kabisa au kukuibia haki yako. 

Unadhani ninikitatokea baada ya hapo? Ni sababu namba nne hapo chini.


Kuvunjika kwa ndoa / mahusiano

Hakuna mwanamke anaweza kuvumilia kukaa na mwanaume ambaye hamridhishi. Atavumilia lakini mwisho atachoka. Asipovunja mahusiano yenu basi atakufanya wewe uvunje mahusiano au ndoa hiyo.


Mbali na hayo, madhara mengine ni pamoja na;-

 • Hasira za mara kwa mara kwa mwanamke
 • Kusababisha ugonjwa wa moyo kwa mwanamke kwa kutofikishwa kileleni
 • Mwanamke kubaki na maumivu wakati wa tendo la ndoa
 • Mwanamke kuchukia tendo la ndoa
 • Kukosa usingizi

 

Hitimisho

Ingawa hatufanani lakini jitahidi kadiri ya uwezo wako kuhakikisha unakamilisha vema na mwenzi wako tendo hili la asili na la uumbaji wa Mwenyezimungu. Ukimbiwe kwa sababu nyingine lakini sio kwa shoo mbovu.

Uwe na siku njema ndugu msomaji

TUNAKUPENDA

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: TATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI NA SULUHISHO LAKE
TATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI NA SULUHISHO LAKE
Pa pa pa, ndani ya sekunde 30 - dakika 1 mzee ushamaliza. Unaiona dunia yote imekuelemea na hujui cha kufanya. MAKALA HII NI MSAADA KWAKO
https://1.bp.blogspot.com/-E1YfguoM-80/YQfNZM4oR8I/AAAAAAAAh4E/l5gDpCyhCSY8KwM17SGtCSw8vQPmWV7wQCLcBGAsYHQ/s320/images.jpeg
https://1.bp.blogspot.com/-E1YfguoM-80/YQfNZM4oR8I/AAAAAAAAh4E/l5gDpCyhCSY8KwM17SGtCSw8vQPmWV7wQCLcBGAsYHQ/s72-c/images.jpeg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2021/08/tatizo-la-kuwahi-kufika-kileleni.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2021/08/tatizo-la-kuwahi-kufika-kileleni.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content