Nifahamu

Jina kamili naitwa Saidi Rashidi Bunduki. Nilizaliwa mwaka 1989 mwezi wa 10 tarehe 12 siku ya alhamisi saa mbili usiku. Nilizaliwa katika kijiji cha Mkalamo katika wilaya ya Pangani Mkoa wa Tanga - Tanzania.

Ni mtoto wa tatu kuzaliwa na ni mtoto wa pekee wa kiume kwa sasa katika familia ya Sheikh Rashidi Saidi Samfyomi Bunduki. Huyu ni Sheikh mkuu katika kijiji chetu cha Mkalamo. Kama humfahamu unaweza kubonyeza HAPA

Nilianza elimu ya awali (chekechea) mwaka 1997 na elimu ya msingi mwaka 1998 na nilimaliza mwaka 2004 darasa la saba na kufaulu kuelekea katika shule ya sekondari ya kutwa iliyoko mjini Pangani ambayo hujulikana kama Funguni Sekondari. 

Nilimaliza elimu ya sekondari mwaka 2008 kidato cha nne na baada ya hapo sikuweza kuendelea tena na masomo. Nilirudi Kijijini kuendelea na elimu ya dini.

Mwaka 2012 nilipata mafunzo ya kozi fupi ya Kompyuta mjini Pangani na baada ya mafunzo hayo ya miezi minne nilibahatika kupata kazi katika moja ya stationary zilizoko Pangani mjini. Nilifanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja na miezi mitatu. Mwaka 2014 nilirudi tena Kijijini kuendelea na kufundisha elimu ya dini pamoja na kufanya kilimo kidogo.

Mwaka 2015 nilipata tena fursa ya kwenda jijini Arusha kwa ajili ya kupata tena mafunzo ya Kompyuta katika Kampuni moja ambayo ilikuwa inajihusisha na uuzaji wa Kompyuta, Printer, fotokopi pamoja wino zake. 

Mwaka 2016 niliajiriwa rasmi katika Kampuni ile katika tawi lake lililoko jijini Mbeya.

Nilioa mwaka 2016, mwezi wa 12, tarehe 30 na mpaka sasa nina watoto wawili (wakiume na wakike).

Nilipata mafunzo ya udereva mwaka 2020 mwezi wa kwanza katika shule ya GM DRIVING SCHOOL iliyoko mtaa wa SINDE jijini Mbeya na kumaliza rasmi mwezi wa tatu. Nilitunukiwa cheti cha udereva na baadaye kupata leseni kutoka mamlaka ya mapato tanzania T R A.

VITU NINAVYOPENDA
  1. Kusoma na kuhifadhi Qur an
  2. Utunzi na uandishi wa mashairi ya kiswahili
  3. Utunzi na uimbaji wa kaswida
  4. Uandishi wa makala mbali mbali
  5. Kusoma hadithi, visa kutoka katika blog mbali mbali
  6. Kujifunza mengi dhidi ya Utunzi na uandishi

Lakini pia mimi ni BLOGGER mchanga ambaye najihusisha na maudhui ya fasihi zaidi na makala za afya.

Karibu katika blog yangu kujifunza zaidi. Bonyeza anwani hii hapa chini

HII NI HISTORIA YANGU KWA UFUPI

ASANTE.Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
static_page
mrbunduki: Nifahamu
Nifahamu
Nifahamu japo kwa uchache.
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/p/historia-ya.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/p/historia-ya.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content